“Kujaribu sio kushidwa” Binti Tumalumbage Baraka Boniface ambaye ni mwafunzi wa stashahada ya Biomedical Laboratory technology kutoka nchini Tanzania anasoma chuo kikuu Makerere kilichoko Kampala Uganda.”
Tumalumbage ambaye ni mwanafunzi anasema kusoma darasani kwake ilikuwa haitoshi bali alijifunza mbinu za kufanya ujasiliamali kwa kutumia mikono na fani tofauti kupitia mitandaoni na wakati mwingine aliweza kuudhuria semina za ujasiriliamali.
Kupitia ujuzi wa ujasiliamali wote aliopata katika semina na mitandaoni aliamua kutengeneza viatu aina ya sandozi(ndara) za kitamaduni (viatu vya kimasia). Kama binti kike mahitaji uongezeka kila wakati katika Maisha ya kawaida,Tumalumbage Baraka anasema pesa ya matumizi wazazi waliokuwa wakitumia bado ilikuwa haikidhi maihitaji yake yote na hapo ndio alipopata wazo la kuanzisha biashara hiyo.Alitafakari wapi atapata mtaji ndipo aliona kupitia pesa ya matumizi anayotumiwa na wazazi wake anaweza kufanya biashara na hikampatia pesa inayoweza kukidhi mahitaji yake yote.
Kabla ya kuanzisha ya biashara ya kutengeneza na kuuza viatu vya kitamaduni,mwaka jana 2021 mwezi wa 10 ,alianzisha biashara ya kuuza juice kwa wanafunzi, ambayo kupitia faida aliweza kuzalisha katika biashara hiyo aliweza kuanzisha biashara nyingine ya kutengeneza viatu vya kitamaduni (viatu vya kimasai) kwa kianzio cha shilingi laki moja tu ya kiganda.
Siku zote mwanzo huwa mgumu,anasema alichukua pesa hiyo na kununua vifaa na mahitaji yanayohitajika kutengeneza viatu vya kitamaduni, alianza kutengeneza japo kulikuwa na ugumu kupata wateja na kumgharimu kutembea na bidhaa hizo katika maofisi mbalimbali mjini kamapla na hata kwa wanafunzi wenzake kupata wateja na kupitia njia aliweza kupata wateja baadhi.
Ushauri ujenga, kwani aliweza kupata ushauri kutoka kwa wateja na watu wengine juu ya utengenezaji wake wa viatu hivyo, kupitia ushauri huo ndio ulikuwa mwanzo wa kujijenga katika biashara na kufanya vizuri Zaidi katika utengenezaji wa viatu hivyo kuwa bora Zaidi. anasema anaweza kutengeneza viatu 40-500 na inategemea mteja uhitaji viatu vingapi.
Anasema katika kukuza biashara changamoto hazikosi, kwani muda wa masomo na huku wateja wakihitaji viatu inakuwa vigumu na wakati mwingine, pia wateja wengine uchukua kwa mkopo na kuchelewa kulipa kwa wakati lakini kupitia changamoto hizi sio chanzo cha kunirudisha nyuma hadi sasa nimekisha zipatia ufumbuzi na biashara hii ni endelevu na inaendelea kukua Zaidi.
Kijana wa sasa mikono yako yaweza kuleta mafanikio makubwa katika Maisha yetu kama vijana endapo utaitumia vizuri katika kazi, biashara na ujasiliamali wa kutengeneza kitu au vitu kitacholeta faida na maendeleo kwako na kwa jamii kwa ujumla.