Moja kati ya hamasa ya vijana walio vyuo vikuu sio kuelimika tu, laa hasha! Ni kuhitimu na kumiliki kazi yenye kuwapa uhakika wa kujitegemea.
Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, mwaka 2015, theluthi moja ya vijana milioni 420 wa Afrika kati ya miaka 15 na 35 hawakuwa na ajira wakiwemo wahitimu na wengi wao huishia mitaani kwa kukosa kazi au ajira.
Wasomi wamekuwa wengi ila ajira ni chache na vijana kushindwa kujiongeza katika eneo la kujiajiri. katika hali hiyo wapo vijana ambao wametumia mafunzo yao walio pata shuleni na vyuo vikuu kujiajiri ili kujitengenezea ajira.
Boniface Mchunguzi, ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere kilichopo jijini Kampala nchini Uganda, anayesoma stashahada ya udaktari wa mifugo. Kupitia mafunzo hayo aliamua kuepuka umaskini na kuwa mfanya biashara na mjasiriamali kwa njia ya usindikaji wa maziwa ya mtindi mzito pamoja na maziwa lala.
Kila kilicho msukuma kijana Boniface katika ujasiriamali ni mahitaji yake kuwa mengi kuliko uwezo wake na hata wazazi na ndugu zake kushindwa kutimiza, ndipo mnamo mwaka wa 2021 aliamua kuanzisha biashara yake inayoitwa “Freyo Fresh Yoghurt”
Akiwa na wenzake kadhaa ambao walichangia kwa asilimia kadhaa ili kuunda kikundi kiitwacho “Dream investment club.”
Boniface anaeleza kwamba biashara ya kutengeneza maziwa lala pamoja na mtindi mzito yeye na wenzake wanatumia mikono yao na vifaa vya kawaida kama ndoo ambazo zinatumika kuchanganya maziwa na viungo vingine, madumu ya kutunza maziwa na vifaa vingine zaidi ili kuzalisha na kuaanda maziwa lala na maziwa mtindi mzito. Kwa mchakato huo, wanafuata vigezo vya kuzaliwa maziwa salama kwa wateja wao.
Bidhaa hii ya “Freyo Fresh Yoghurt” ni ya tofauti sana kwani hutumia maziwa ya asili ng’ombe na hutumia viungo yenye gharama na bora aina ya stabilizer, cultures na favouries, vinavyopatikana katika kampuni ya Promarco na hapo huyasindika na kutoa maziwa mazito yenye ladha tofauti pia, baada ya kuzalisha maziwa hayo huyapakia katika madumu yenye vipimo tofauti ya lita tano hadi tatu na 500ml zote zinapatikana kwa bei nafuu.
Kampuni ya“Freyo Fresh Yoghurt” ina bidhaa ambayo inatengeneza na pure Extress inayotokana na maziwa wanayosindika ni ya ladha nzuri sana na kwa wale wanywaji maziwa mtindi wazoefu wanaweza kuhisi ladha tofauti na kufanana kabisa na yale yanayotoka viwandani.
Waswahili husema “mshika mbili moja humponyoka” lakini kwa kijana Boniface msemo huu kwake haufanyi kazi, Boniface anasema yeye huanza vipindi saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. lakini kwake amekuwa akitumia muda vizuri kukamilisha kila kitu kwa wakati anasema huletewa maziwa saa 12 Alfajiri na hapo uanza kusindika na kuacha maziwa maziwa hayo masaa 6 – 10 kuganda ambapo hadi kufika saa 11 za jioni anaporudi nyumbani kwake tayari yako tayari kuyakoroga na kuyapakia kwa vifaa husika.
“Freyo Fresh Yoghurt” kiwanda cha usindikaji wa maziwa lala pamoja na mtindi nzito kiko chini ya nembo ya chuo kikuu cha Makerere ambapo maabara ya chuo tayari imechukua vipimo vya bidhaa zetu, tukisubiri ndipo tutakuwa rasmi tumehalishwa na mamlaka ya viwango vya bidhaa (UNBS) kwa kupata cheti cha kumiliki kiwanda hicho,” Boniface anafafanua.
Ama kweli kijana ni maji ya moto, kwa maana kwamba kijana hupenda kujaribu kila kitu kinachokuja mbele yao katika kujaribu jambo. Kama kijana ni vyema kuangalia jambo hilo linaleta faida kwako au hasara na katika kujaribu na kufanya jambo kunahitaji pesa kwa kiasi fulani na muda wako.