Viongozi mbalimbali wakiongozwa na balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Azizi Mlima pamoja na wanafunzi Watanzania kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Uganda wamejitokeza katika uwanja wa Julius Nyerere Leadership Centre (JNLC) katika chuo kikuu cha Makerere katika kumbukizi ya miaka 100 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere.
Akihotubua umati mkubwa wa waliohudhuria hafla hiyo, Dkt. Azizi alisema, “ Siku hii ni muhimu kwa sababu mwalimu alikuwa bingwa wa ukanda wa Kusini mwa Afrika na alikuwa na falsafa ya kujitegemea katika bara la Afrika. Huku aliongeza kwamba, “alikuwa bingwa wa elimu kwa sababu wakati wake, alihakikisha kwamba wanafunzi wanaweza kutoka shule ya msingi hadi Chuo Kikuu na kusomeshwa bure kwa sababu sio kila mtu anatoka katika malezi yakati.”
Aidha aliongeza kwamba mwalimu alifanikiwa kuibadilisha nchi kwa njia hiyo pamoja na kuwa mpigania uhuru, ukombozi Kusini mwa Afrika. Itakumbukwa kuwa nchi nyingi za Kusini mwa Afrika zilip
ata uhuru kwa sababu ya juhudi za mwalimu na wengine walijichukulia wenyewe kwamba ni Waafrika wenye jukumu la kuwakomboa Waafrika wengine.
Mwalimu Julius Nyerere, kutokana na mchango huo, tunasherehekea maisha yake leo. Ikiwa angekuwa hai, angeweza kugeuka miaka 100 iliyopita. Na pia alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere.
Na vuguvugu hilo lisiloegemea upande wowote lilikuwa ni kamba ngumu ambapo nchi ambazo hazijaendelea, zingeweza kutembea ili kuhakikisha kwamba hazianguki katika mtego mwingine wowote wa Mashariki au Magharibi wakati wa Vita Baridi. Hivyo nchi zingeweza kuwa huru kuamua wanachofikiri ni maslahi yao kutoonewa kuruhusiwa na mamlaka wakati huo.
Hivyo Mwalimu alikuwa na mchango huo katika mazingira hayo ya kimataifa.
Balozi wa Tanzania Uganda Dkt. Azizi Mlima alitoa Tuzo kwa baadhi ya vyombo vya habari na waandishi wanaofanya bidii kueneza lugha ya Kiswahili nchini Uganda wakiwemo Monday Akoye wa Shirika la utangazaji la Uganda UBC, Issac Mumena mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC pamoja na mwaandishi wa vitabu Profesa mashuhuri nchini Uganda Austin Bukenya, Baada ya kutunikiwa tuzo, Profesa Austin alisema.
Katika tukio la miaka 100 ya kumkumbuka Julius Nyerere hili liliwapatia wanafunzi wa chuo cha Makerere fursa ya kusherehekea pamoja na mzalendo, shujaa na kiongozi anayeheshimika zaidi barani Afrika na mhitimu wa chuo hicho kikongwe.
Pia kulikuwa na kutazama video zilizoratibiwa za mwalimu Nyerere ,vyakula vya Kiswahili, kuvifurahia vitu mbalimbali vya asili vya kitanzania Zaidi ikiwemo kusikiliza muziki , kusoma mashairi na kutumbuiza nyimbo binafsi kutoka kwa wanafunzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kutazama onyesho la ngoma la kizanzibari.
Kiongozi na mwalimu hayati Julius Nyerere amebaki kuwa kumbukumbu ambayo ni vigumu kung’olewa kwenye mioyo ya vijana nchini Tanzania na wa bara lote la Afrika.
Kila mwaka kumeteuliwa siku maalum ya kumkumbuka na kukumbuka mengi mazuri aliyoiachia nchi yake Tanzania na Afrika.
Kati ya wanafunzi waliweza kuhudhuria na kushiriki ni wanafunzi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda ambao walipewa nafasi ya kushiriki mashindano ya kuongea na kuandika lugha ya Kiswahili huku wengine wakitunukiwa zawadi za kufanya vizuri.
Nukuu za hayati baba wa taifa zikiendelea kukumbukwa na kuenziwa kwa kufanyiwa kazi hasa vijana tutaona viongozi bora Afrika na mashujaa wakiwa wazalendo wa nchi zao katika Afrika Mashariki na bara lote la Afrika.