“Kitunze kidumu” ndivyo wasemavyo waswahili, msemo huu umeleta maana halisi na kudhihirika wazi mara tu baada ya Chuo kikuu cha Cavendish nchini Uganda kutumia utalii wa ndani kwa lengo la kuufahamu mji wa Kampala na vivutio vyake pamoja na kuhakikisha wanawapatia wanafunzi wageni na wenyeji fursa ya kukutana na kufahamiana.
Wakati huo huo, wanafunzi hao wakichukua fursa hiyo kubadilishana mawazo kwani kwa miaka miwili iliyopita hawakuwai kuonana ana kwa ana na walimu wao au hata wenyewe kwa wenyewe kutokana na janga la Uviko-19.
Lakini kwa kuwa kilio cha wengi husikika kwa haraka, mnamo tarehe 16 Desemba 2021, Waziri wa Elimu, Janet Kataha Museveni, alisema shule zote na taasisi nyingine za masomo zimeratibiwa kufunguliwa Januari 10, 2022. Hadi kufikia sasa ni wiki ya tatu siku kadhaa kufika mwezi moja tangu kufunguliwa rasmi kwa ratiba ya masomo ya mwaka huu.
Mnamo February 3, 2022 Uongozi wa Chuo Kikuu cha Cavendish uliaanda siku makhsusi ya ziara ya utalii wa ndani chini ya kauli mbiu “Wiki ya ajabu” ambapo wanafunzi wa chuo hicho walitalii ndani ya mji wa Kampala Uganda, ilikuwa ni njia ya kusema karibu Cavendish! Kwa wanafunzi.
Kiongozi wa Chama cha chuo kikuu cha Cavendish Blessed Atwine Mugisha anasema kwamba lengo na madhumuni ya ziara hiyo ya “wiki ya ajabu” na utalii wa ndani ni kuwawezesha wanafunzi wa kigeni na wenyeji kufahamu kwa undani mji wa Kampala na maeneo yake ya Kihistoria.
Kampuni ya Kiasightseeing wakishirikiana pamoja na chuo hicho maarufu walizitia tabasamu nyuso za wanafunzi na kuzijaza furaha nyoyo zao huku wengine wakipigwa na butwaa baada ya kutembelea kasri ya mfalme wa Buganda almaarufu Kabaka iliyoko Mengo, ziwa la Kabaka linaoshikilia rekodi ya ziwa kubwa zaidi nchini Uganda liliochimbwa kwa kutumia mikono, Lubaga Cathedral ambayo ni Mapapa watatu, Chuo kikuu cha Makerere, Hospitali ya Lubaga pamoja na uwanja wa uhuru unaopatikana Kololo.
Kabula Deogratis mwanafunzi kutoka Tanzania aliye mwaka wa kwanza anasema, “nimefurahi sana kufanya ziara hii na kama ningekosa ningeumia sana, maana ni mara yangu ya kwanza kutembea na kuliangalia jiji la Kampala. Nilichofurahia ni usafiri ulikuwa ni mzuri sana maana hayo mabasi ya aina mbili sikuwa kupanda na huduma tulizopata kutoka waongoza utalii kutueleza historia za maeneo husika ambapo mimi sikuwa nafahamu milima saba ya kukamilisha jiji la kampala, na nilivutiwa sana na ziwa la kabaka ambalo liliundwa kwa kutumia mikono.
Aidha aliipa pongezi za dhati Radio ya MCI akiongeza kwamba, “MCI Radio iko juu sana kwa sababu inatoa huduma mbalimbali bure mfano picha,mahojiano na burudani za hapa na pale ni tumia lugha mbalimbali hivyo inasaidia kufikiwa kwa watu wote hakika nimeipenda mno.”
Ama kweli vyuo vyote nchini Uganda vikitumia ziara kama hii au njia zingine za kuwashawishi na kuwavutia wanafunzi wageni hasa baada ya kipindi kirefu pasi na masomo, inaweza kuwashawishi wanafunzi hasa wale wanaomaliza masomo ya shule za upili kuvutiwa kujiunga na vyuo mbali mbali na pia ni moja ya njia ya wanafunzi wenyeji kupigia debe vyuo.
Story by Faima Ibrahim