Chuo kikuu cha Makerere kimeadhimisha miaka 100 ya uongozi wa Julius Nyerere moja ya vituo maarufu
vya uongozi katika taasisi hii ambayo ilianzishwa kwa kutambua urithi wa Uafrika uliowekwa na
aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Wageni kutoka mataifa 12 wanahudhuria maadhimisho hayo yenye lengo la kuenzi mchango wa kiongozi
huyu wa kitaifa ambaye utendaji wake na sifa zake zilitambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kongamano hilo liko chini ya mada “Mustakabali wa Kiafrika unaoongozwa na Vijana wa Afrika”.
Shughuli zinazohusika katika kongamano hilo ni pamoja na mazungumzo kati ya vizazi juu ya uongozi wa
vitendo, shughuli za kitamaduni za kusisimua na midahalo shirikishi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Barnabas Nawangwe alisema, “Si
ajabu kwamba Mh.Rais Kaguta Musevene aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha Makerere alijivunia sana
kuwa na Mwalimu Nyerere ndipo aliona ni vyema kuanzisha Kituo cha Uongozi cha Julius Nyerere katika
Chuo Kikuu cha Makerere ili kuendeleza mambo ya mwalimu wake,”
Waziri wa mambo ya ndani, Kahinda Otafiire aliyekuwa mgeni rasmi,kumwakilisha Rais Yoweri Kaguta
Mseveni alisema katika kongamano hilo “Ni lazima tuwe na mjadala kuhusu kuacha kuwa Waganda na
tuwe Waafrika. Tunahitaji kuhangaika sana kumaliza suala la mapambano ya ukombozi wa Afrika ambayo
sasa yameegemea kwenye uhuru wa kiuchumi pia Nyerere hakuwa sehemu ya klabu yako ya kucheza
dansi, alikuwa mwanafalsafa aliyeielewa dunia na kuthamini utu. Kama Waafrika, tunapaswa kuepuka
yale yanayotugawa na kuzingatia yale yanayotupatanisha sisi. Alimalizia kwa kusema lazima tukumbatie
itikadi za mwalimu julius nyerere na tusonge pamoja kama Afrika.
Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Mhe. Aziz Mlima, naye aliweza kuzungumza na kusema “ vijana wa
leo wanapaswa kuwa bingwa wa masimulizi matatu katika uhuru wa Julius Nyerere; ukomboaji wa akili
zao na kuwa na uhuru wa kiakili ,Utafiti, Ubunifu na uhuru wa uvumbuzi katika Elimu kwa uhuru wa
teknolojia.
Moja ya wajumbe kutoka nchini South Afrika Dk. Eddy Maloka, Mtendaji Mkuu wa Africa Peer Review
Mechanism alisema kuwa Historia ya Makerere inaakisi historia ya harakati za kupigania uhuru kwa
mataifa mengi ya Afrika pia Historia ya Makerere ni Historia ya Afrika. Makerere amefungua milango
yake kuwa nyumbani kwa waandishi wengi Maarufu kama Ngugi wa Thiongo John Nagenda, Timothy
Wangusa, Okot pr Bitek miongoni mwa wengine," Dkt. Makola alisema.
Mzee Joseph Butiku, mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi alitoa matumaini kwa vijana kwani
mustakabali na ushirikiano wa Afrika ni wao. Hata hivyo aliwataka wajifunze kutoka kwa wazee ambao
wameweka msingi imara wa uafrika. "Ninawaomba vijana wasome historia ya wazee tangu kuwa msingi
wa kubadilisha Afrika. Historia inakupa fursa ya mazungumzo kuhusu masuala ya Afrika," alihimiza.
Katika kongamano hili vijana kutoka nchi mbalimbali waliweza kualikwa kama Kijana Gabriel Karsan
kutoka Tanzania ambaye ni muhamasishaji wa vijana katika sekta ya interneti alisema “kuna mengi
yaliopita ambayo yapo na yanayofuata lakini ni misingi ambayo wote tunayo, nia moja ni kutengeneza
Afrika ambayo inajumika kwa pamoja na inajengwa kwa watu.
Katika nukuu za Mwalimu Nyerere pindi alipokuwa akihutubia palipo vijana aliwai kusema “Tunataka
kuona vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya kidhalimu isiyoshabihiana na rnatakwa na
matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika
Taifa.
Sangu Bukiku Afisa Msaidizi wa Mipango katika Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Tanzania) kama
mwalikwa naye alisema anayo furaha ya kuona vijana wengi walioshiriki kongomano hili lakini pia
ninaona tumaini Afrika, naona waafrika wadadisi wanapenda kuuliza kwanini.
Sophia maka kutoka nchi Tanzania na mkuu wa maktaba na nyaraka za kihistoria naye alisema “ alifurahi
kupata mwaliko wa kufika nchini Uganda kwa kusherekea na kuadhimisha miaka 100 Makerere na
Nyerere kwani katika kongomano hili nijufunza vijana wanapaswa kuendeleza urithi wa waasisi wetu
kama waafrika na alitoa ushauri vijana wajifunze urithi kupitia midahalo kwa wingi na kuzungumza.
Mwalimu Julius Nyerere ataendelea kumbukwa kwa mambo mengi mazuri aliyoiachia nchi yake Tanzania
na Afrika kwa ujumla , ukiwemo umoja na mshikamano na amani miongoni mwa Afrika pamoja na
kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa watu wa Afrika
Hii leo nchini Uganga na Afrika mashariki kwa ujumla wanaadhimisha miaka 23 ya kifo cha baba wa taifa
hilo, lakini bado Falsafa zake zinaendelea kuishi kwa wazee na vijana maana ndio taifa la sasa.